All Library resources are free to download, use and remix (learn more)

Jinsi ya Kuweka Kumbukumbu Wakati Mtandao Umezimwa Jinsi

Kuweka kumbukumbu za ukiukwaji wa haki za binadamu ni muhimu kama ilivyo kawaida  hata wakati mtandao umezimwa. Hata kama taarifa hazita sambazwa muda huo, kuchukua kumbukumbu  kutakuwa njia ya kuhifadhi zile sauti ambazo mamlaka zinataka kunyamazisha, na kuweka ushahidi wa dhuluma ambazo zitakuja kutumika kama kidhibiti baadaye katika kuwawajibisha. Hata hivyo, ukandamizwaji na vikwazo vya kiteknolojia vya kuzimwa kwa mtandao hufanya kuchukua kumbukumbu za ukiukwaji na utunzaji wake kiusalama kuwa na changamoto na hatari. Wanaharakati watawezaje kunasa na kuhifadhi video zao wakati mtandao umezimwa, na hata kusambaziana video hizo bila mtandao, na kufanya hivyo kwa njia salama?

Kupitia kazi zetu na wanaharakati ambao wana uzoefu na uzimwaji mtandao, tumejifunza vitu muhimu na jinsi ya kunasa na kuhifadhi kumbukumbu za video wakati mtandao umezimwa ambao tuta shirikishana kwenye mfulululizo huu. Tuliandika kwa kuangazia vifaa vya Android zaidi, japokuwa vitu hivyo vinaweza kutumika kwenye iPhones pia. Mikakati baadhi inahitaji maandalizi ya mapema (na mara nyingi, kuwa na mtandao), hivyo basi ni wazo zuri kuhakiki na kutekeleza hatua zozote zile kabla ya kujikuta katika mazingira ambayo hauna mtandao na unataka kuchukua kumbukumbu. Weka nakala mojawapo ya mafundisho ambapo utapitia au kusambaza  wakati mtandao umezimwa. Na mwisho, anza kufanyia mazoezi mbinu na njia hizi katika shughuli zako za kila siku ili ziwe sehemu ya pili ya kawaida  ya maisha yako kabla hujapitia katika hali mgogoro.