Kusambaziana Faili na Kuwasiliana Wakati Mtandao Umezimwa
Uzimaji mtandao unalenga kuwazuia watu kusambaziana taarifa na kuwasiliana (na pia kulazimisha watu kuwa katika hali ya mawasiliano yasiyo salama sana kama vile simu za mkononi na meseji, ambavyo ni rahisi kwa mamlaka kuingilia na kufuatilia). Kamwe hakuna mbinu nzuri za kutafuta suluhu wakati mtandao umezimwa kabisa.
Hatuna njia ya uhakika kabisa ya kuweza kukwepa vizuizi vyote, lakini kupitia mazungumzo na wanaharakati na wenzetu, tumejifunza baadhi ya mbinu na njia za kutumia kwa ajili ya kusambaziana na kuwasiliana zinazoweza kukusaidia wewe, kulingana na hali na mazingira. Kumbuka kuwa baadhi ya njia hizi huhitaji mtandao awali ili kuweza kuseti (mfano, kupakua aplikesheni).
Collection(s) | All resources |
---|---|
Region/Country | Africa |
Topic(s) | Internet Shutdowns, Mobile Phones, Safety & Security Planning, Transferring Files |
Type | Tipsheet |
Language | Kiswahili |