Kuseti Simu kwa Ajili ya Kuweka Nyaraka Wakati Hakuna Mtandao

$0.00

Description

Licha ya kuzimwa kwa mtandao, wachukua nyaraka bado wanaweza kunasa ushahidi muhimu wa video unaoweza kusambazwa bila kuwa na mtandao au watakapo pata mtandao.

Hivi hapa ni baadhi ya vidokezo ambavyo tumejifunza kutoka kwa wanaharakati na watendaji wengine kuhusu jinsi ya kuseti simu kuchukua nyaraka wakati hakuna mtandao. Kumbuka kuwa baadhi ya hatua zitahitaji uwe na mtandao, hivyo lazima zifanyike kabla mtandao haujazimwa
au wakati mtandao utakapo rudi. Pia, usisubiri hadi uwe katika hali ya taharuki ndio uzingatie hatua hizi; zifanye sasa, na tafuta muda ufanye mazoezi ya kutumia simu kabla ya kuhitaji kutumia wakati wa migogoro.

Help WITNESS create more human rights change

Join us by subscribing to our newsletter.

Support WITNESS