Naweza Kutumia Aplikesheni hii ya Kuweka Nyaraka?
Kuna aplikesheni nyingi ambazo wachukua nyaraka wanaweza kutumia kwa kunasa video, ambapo inaweza kuwa ni aplikesheni ya kamera ya simu yako, aplikisheni maalum kwa ajili ya kuchua nyaraka kama vile ProofMode, Tella, au Eyewitness to Atrocities. Baadhi ya aplikesheni zina vipengele vinavyo tegemea mtandao, hivyo ni vema ukakumbuka kuwa vipengele hivyo havitakuwepo ikwa mtandao utazimwa.
Hatuwezi kukuambia ni aplikesheni ipi itakufaa wewe, kwa kuwa hilo lina tegemeana na hali yako, mahitaji yako, na hatari zilizopo (angalia makala hii kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kupima migogoro na hatari). Ukiwa na tathmini ya hatari zilizopo mkononi, haya maswali ya mwongozo hapa chini yanaweza kukusaidia kutathmini ni aplikesheni ipi ya video inayoweza kuwa nzuri zaidi kwako.
Collection(s) | All resources |
---|---|
Region/Country | Africa |
Topic(s) | Internet Shutdowns, Mobile Phones, Safety & Security Planning, Transferring Files |
Type | Tipsheet |
Language | Kiswahili |